Msanii Nandy amesema changamoto kubwa katika muziki wake kwa sasa ni kuhakikisha anaendelea kuwa juu huku akimtaja Maua Sama kuwa ni miongoni mwa msanii ambao anawachukulia kama washindani wake wakubwa katika muziki.
“Yaani nikija kutoa wimbo usishuke au uwe juu zaidi, au nifanye ubunifu gani kutofautiana na wenzangu ili niweze kubakia katika nafasi yangu. Wasichana wote kwenye industry wapo katika ushindani kwa sababu tunafanya biashara moja, kwa hiyo ninapomuangalia mtu kama Maua namuangalia kwa jicho la kama msanii mwenzangu, kwa jicho la kibiashara, kwa hiyo namuangalia kama mshindani wangu,” ameeleza Nandy.
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments