Saturday, May 27, 2017

thumbnail

RC Makonda apokea Mwenge wa Uhuru Dar


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi (Kulia) katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda Leo Me 27, 2017 amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi katika dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma na kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke tayari kwa kumulika miradi ya Maendeleo.

Mara baada ya kukagua Miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Temeke Mwenge wa Uhuru utazuru katika Wilaya ya Kigamboni Tarehe 28/05/2017, Siku ya Tarehe 29/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ilala, Tarehe 30/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Kinondoni na Tarehe 31/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ubungo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amesema kuwa Mwenge wa uhuru ni chombo kilichoasisiwa na baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni Tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika hivyo kuzuru katika Mkoa wa Dar es salaam itakuwa ni kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo, Uzalendo, Umoja , Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya Taifa letu.

Mhe Makonda alisema kuwa Mwaka huu utakuwa mwaka wa 24 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe chini ya utaratibu wa usimamizi wa serikali kutokana na mabadiliko ya kidemokrasia baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

Katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya Mhe Makonda alisema kuwa jitihada ya kudhibiti kusambazwa na Matumizi ya Dawa za Kulevya ni kuifanya kuwa ajenda muhimu kiutekelezeji kwa mustakabali wa maisha ya watanzania kwa kuwa Jambo hilo linagusa nguvu kazi ya Taifa. 

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music