Tuesday, June 20, 2017

thumbnail

Aliyetaka kuinginza nyama gerezani afahamika


Ramadhan Nombo, mkazi wa Jiji la Dar jana amenaswa na askari magereza katika Gereza la Mahabusu la Keko akitaka kuingiza simu tano.

DAR ES SALAAM: Kijana mmoja, Ramadhan Nombo, mkazi wa Jiji la Dar jana amenaswa na askari magereza katika Gereza la Mahabusu la Keko akitaka kuingiza simu tano alizokuwa amezificha ndani ya mapande ya nyama yaliyorostiwa. Tukio hilo la ajabu limetokea jana baada ya Nomba kuwapelekea ndugu zake chakula.

Kwa mujibu wa chanzo, Nombo alipanga kuingiza simu tano ambazo alizipachika kwenye mapande ya nyama iliyorostiwa kisha kuwapelekea ndugu zake walioko gerezani hapo.  Hata hivyo, haikufahamika alikuwa anawapelekea kwa sababu gani, na wafungwa wa kesi zipi.

Mtandao huu ulimtafuta Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, ASP Lucas Mboje ili kuzungumzia tukio hilo ambapo alikiri kutokea na akaelekeza aonwe Mkuu wa Magereza wa Dar.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, DCP Augustine Mboje alipoulizwa alisema ni kweli kijana huyo amekamatwa.

Kama akikutwa na hatia atakuwa amevunja Kifungu cha 86 (1) cha Sheria za Magereza sura ya 58 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, inakataza kwa mtu yeyote kuingiza kitu chochote kisichoruhusiwa gerezani na atahukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita(6) au faini au vyote kwa pamoja.

Hadi sasa Nombo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music