wa Bongo Fleva, Timbulo amesema ni kweli muziki wake umevuna
mashabiki wengi kutoka kwenye kundi la warembo kutokana na tungo na
muonekano wake pia.
Mwimbaji huyo ameeleza hata nyimbo zake za awali kama ‘Domo Langu’ zinapelekea hali hiyo na kuongeza hata baadhi ya wanaume wamekuwa wakipenda muziki wake lakini wamekuwa wagumu kuweka wazi hilo.
“Ni kweli si uongo kutokana na aina ya muziki ambao nimekuwa
nikiufanya. Lakini kitu ambacho nakiamnini pia kwa upande wa pili mimi
ni mmoja wa wasanii wakati nilivyoanza mwanzo washikaji wengi sana
walitumia ngoma zangu kwa ajili ya kuwasilisha jumbe zao kwa watoto wa
kike,” Timbulo amekiambia kipindi cha Show Time cha Radio RFA.
“Nikikurudisha nyuma kidogo unaweza kuona jinsi ngoma yangu ya Domo
Zito ilivyoleta matokeo chanya na ilisababisha vijana wengi kuitwa
Timbulo kwa kuwa niliimba sijui kutongoza. Hata kuna baadhi ya wadada
waliwahi kunitumia, sometime unakuta mtu anakuelewa lakini anashindwa
kukuambia,” ameongeza Timbulo.
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments