Hospital ya wilaya ya Kahama
inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vipimo vya ugonjwa wa Kisukari, jambo
ambalo linachangia Wagonjwa wengi kwenda hospital binafsi kufanyiwa vipimo
hivyo.
Akizungumza na Kijukuu Blog ofisini kwake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospital hiyo Dkt FEDRICK MALUNDE amesema tatizo lililopo ni kwamba vipimo hivyo
vikifika huisha mapema kutokana na
wagonjwa kuwa wengi.
MALUNDE amesema watu
wanaohusika na manunuzi wameanza mchakato wa kununua vipimo hivyo ili
kuhakikisha huduma zinarejea kama kawaida ambapo wagonjwa kati ya 40 hadi 50 hufanyiwa vipimo kila siku katika hospitali
hiyo.
Kutokana na hali hiyo MALUNDE
amesema wananchi wanatakiwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki wakati wanafanya
utaratibu wa manunuzi ya vipimo hivyo
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments