Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro jana alifanya mazungumzo na wazee
pamoja na viongozi wa dini wilayani Kibiti mkoani Pwani ili kubaini
waalifu wanaotekeleza mauaji ya watu wilayani humo na kusema vyovyote
itakavyokuwa lazima watawarudisha kwenye msitari.
IGP Sirro
alisema kupitia mazungumzo hayo tayari amepata taarifa za wahalifu hao
ingawa ni mapema kuziweka wazi ila amewakikishia wananchi kuwa waalifu
wao ni lazima watapatikana.
“Kubwa ni
kwamba wazee wetu wa Kibiti wametueleza taarifa nyingi sana na mnavyojua
hawa waalifu wanaishi ndani ya Kibiti, ndani ya Ikwiriri, kwa hiyo
wazee wetu wamejaribu kutueleza ni wapi tunaweza kuwapata na chanzo cha
mambo yote haya,” alisema IGP Sirro na kuongeza;
“Kwa hiyo
kimsingi mambo mengine mengi ni ya kipelelezi ambayo siwezi kuyasema kwa
sasa, lakini kikubwa wametupa dira, muelekeo kwa maana kwamba wale
ndugu zetu au maadui zetu kwa lugha nyepesi tumepata njia nzuri ya
kudeal nao. Kwa hiyo nitume salamu kwao kwamba waendelee kukimbia lakini
njia ya muongo ni fupi na mwisho wa siku tutawarudisha kwenye mstari"
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments