Thursday, June 29, 2017

thumbnail

Kilimo bora cha tangawizi



Utayarishwaji wa shamba.
Kuandaa shamba kwa ajili ya kulima Tangawizi unaweza kutumia trecta, jembe la mkono au la ng’ombe kutayarisha shamba, shamba litayarishwe mwezi mmoja kabla ya kupandikiza kwa kukatua ardhi hadi kufikia kina cha sentimita 30. Lainisha udongo. 


Shamba linatakiwa kuandaliwa vituta vidogo vidogo kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka tuta hadi tuta, hiihusaidia kuhifadhi udongo na maji na hutoa nafasi nzuri wakati wa upanukaji wa viazi. Inashauriwa pia kama matuta hayajatumika basi ni muhimu kujaza udongo kwenye shina kwani pingili za chini kwenye shina ni lazima zifunikwe na udongo ili zitoe viazi kwa wingi na hivyo mavuno huongezeka.

Utayarishaji wa mbegu.
Mbegu iandaliwe mapema mwezi mmoja kabla ya kupanda na pia itunzwe katika mazingira mazuri kwenye kivuli pasipo na jua ikiwezekana weka ndani ya chumba kinachopitisha hewa, pindi unapokwenda kupanda katakata vipande urefu wa nchi moja na hakikisha tunguu haijakauka. Kiasi cha kilo 840-1700 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja.

Upandaji
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Tangawizi humea na kukomaa baada ya miezi 8 mpaka 10. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda.

Kiasi cha kilo 840-1700 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja. Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita. 23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana. Na inahitaji uangalizi kwa matokeo bora.

Mbolea
Weka mbolea za asili zilizooza vizuri kiasi cha ndoo moja hadi mbili, kwa eneo la mita mraba 10. Mbolea hii iwekwe katika kila shimo. Kiasi kinachotakiwa ni kilo moja au kopo moja la Tanbond kwa kila shimo. Hii ni sawa kuweka na tani 10 hadi 20 kwa hekta. Baada ya wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekta na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.


Upandaji.
Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua magugu, kama simazine hutumika. pandishia tuta ili kufanya tangawizi kutunza unyevu na huota vizuri


Magonjwa na wadudu. 
• Madoa ya majani yanayosababishwa na viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.

• Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp • Mizizi fundo; inasababishwa na Meloidegyne spp.
Uvunaji.
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana.

Usindikaji.
Tangawizi ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na sukari na/au chumvi. Hata hivyo tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16.0-18.0%.



Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music