Baada ya Waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa kuitwa na Mkurugenzi wa makosa ya Jinahi (DCI) kwa mahojiano hatimae Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa maelekezo kwa Kurugenzi ya katiba na sheria kuhakikisha wanampatia Mh Lowasa msaada wa kisheria kwenye mahojiano hayo.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Idara ya mawasiliano CHADEMA, Mkuu wa idara ya habari, Tumain Makene amesema Mh. Lowassa amepata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI) jana ambaye amemtaka afike leo saa nne asubuhi bila kupewa maelezo wala ufafanuzi juu ya nini kitajiri katika mahojiano hayo.
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email


No Comments