Tuesday, June 20, 2017

thumbnail

Polisi Dar wazungumzia tukio la Walemavu kupigwa mabomu



Jeshi la Polisi Dar  limekutana na Waandishi wa Habari na kutolea ufafanuzi mambo mbalimbali yaliyojiri na moja kati ya mambo hayo ni swala la  Walemavu waliotawanywa kwa mabomu ya machozi baada ya kuziba Barabara ya Sokoine June 16, 2017 wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa.

Jeshi hilo limesema kuwa halikutumia nguvu kupita kiasi kama inavyodaiwa lakini walitumia nguvu kulingana na watu waliokuwa wakifanya maandamano hayo.

"Hatujatumia nguvu ya kupita kiasi. Tumetumia nguvu kulingana na hali ya watu ambao walikuwa wanafanya maandamano hayo.

"Ulemavu, nataka nitoe rai kwa wananchi ulemavu sio kibali cha wewe kuvunja sheria wala ulemavu haukupi wewe kibali cha kuvunja sheria za nchi. Sheria za nchi zipo kwa mtu yeyote yule – mzima au mlemavu na hasa ambaye anazivunja kwa makusudi akijua.

“Hawa walemavu walifanya makosa, wamevamia Ofisi ya Mkurugenzi  wa Manispaa lakini pamoja na hivyo wakaziba njia. Tumejaribu kuongea nao kuwasihi kwamba wafungue njia lakini pia wateue viongozi wao kwenda kushughulikia matatizo yao lakini walikaidi. Kwa hiyo, ikabidi tutumie nguvu kidogo tukaenda kuwaondosha tukafungua barabara na wananchi wengine wakaendelea na shughuli zao.”

Hayo yalisemwa  jana  na Naibu Kamishna wa Polisi ambaye ni Mkuu wa Operesheni za Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lakini kwa sasa anakaimu nafasi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu kazi mbalimbali ambazo zimefanywa na jeshi hilo.

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music