Tuesday, June 20, 2017

thumbnail

Pwani: JPM awaita wapinzani kwenye mkutano wake


Pwani. Rais John Magufuli ametumia mkutano wake wa kwanza mkoani Pwani kuwataka viongozi wa upinzani ambao wamepokea mwanachama mpya kutoka CCM kutumia mkutano huo kuwatangaza.

Rais alitoa fursa hiyo mara mbili leo (Jumanne) katika mkutano wake wa hadhara  wakati mwanachama wa ACT-Wazalendo aliyehamia CCM alipotambulishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

“Kama kuna mwana CCM amehamia Chadema, aje hapa atangaze, namkaribisha, nipo hapa kuzindua viwanda sijaja kichama lakini nimpishe, nikae pembeni nimuache Katibu wa Uenezi amkaribishe mwana CCM mpya,” amesema.

Hata baada ya mwanachama huyo mpya kutambulishwa na kupata nafasi ya kutoa neno, Rais aliporudi jukwaani na zungumza tena alisema kama wapo viongozi wa Chadema au CUF wamepata mwanachama wa CCM aliyehamia katika vyama vyao, wanaruhusiwa kumtangaza katika mkutano huo.

“Hata kama ni wa CCM amehamia CUF aje atangaze na kama CUF kahamia Chadema, nao pia waje wamtangaze hapa,” amesema.

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music