Wednesday, June 28, 2017

thumbnail

USAJILI: Ngoma amewasili jana usiku- Mkwasa

Mchezaji wa timu ya Taifa ya Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma akiwasili uwanja wandege wa wa kimataifa wa Jk nyerere

Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga SC, Charles Boniface Mkwassa amethibitisha mchezaji wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Zimbabwe, Donald Ngoma ametua nchini usiku wa jana.

Akizungumza na Bongo5 Media, Mkwasa amethibitisha kumpokea Ngoma hapo jana.
“Ni kweli Donald Ngoma ametua nchini jana usiku ila masuala mengine yote tutayaeleza muda utakapo fika”, amesema Mkwasa
Alipo ulizwa juu ya tetesi za mchezaji huyo kuingia mkataba wa miaka mitatu na timu ya Polokwane City kutoka Afrika Kusini Mkwasa alisema, “hata sisi tumesikia hilo ila subiri mpaka tutakapozungumza naye tutayaeleza”.
Kwa mujibu wa mtandao wa KICKOOF.COM, umesema usajili wa mchezaji huyo umekamilika kujiunga na klabu ya Polokwane City huku mkataba na klabu yake ya Yanga unatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni .
Ngoma mwenye umri wa miaka 27, anahusishwa kuwasili nchini jana usiku kwaajili ya kufanya mazungumzo ya kuingia kandarasi mpya na klabu ya Yanga huku Simba nayo ikihusishwa katika mbio za kumsajili mchezaji huyo licha mpaka sasa kutokuwepo na taarifa rasmi kutoka Simba.
Polokwane City wameripoti kuinasa saini ya Ngoma lakini mchezaji huyo amesema yupo kwenye mazungumzo nao kama ilivyo kwa timu nyingine ikiwemo Yanga.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu cha klabu hiyo ya City imethibitisha Ngoma kuingia kandarasi ya miaka mitatu na alikuwa hapo kwaajili ya vipimo.
BY HAMZA FUMO

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music