Shirika
la Afya Duniani (WHO) limesema watu 7.2 milioni sawa na asilimia 80
hufariki dunia kila mwaka duniani kutokana na matumizi ya tumbaku.
Taarifa
iliyosomwa leo na mwakilishi wa mkurugenzi wa WHO nchini, Neema Kileo
inaonyesha kuwa watu 146,000 wenye umri chini ya miaka 30 hufariki
dunia barani Afrika kutokana na magonjwa yanayotokana na matumizi ya
tumbaku.
"Magonjwa yanayouwa zaidi kutokana na matumizi ya
tumbaku ni pamoja na saratani ya mapafu, kisukari, magonjwa sugu ya
mapafu, kuzaa watoto njiti, na kuharibika kwa mimba kwa mama mjamzito"
amesema Kileo
Pia amesema watu 600,000 ambao si watumiaji wa
sigara hufariki dunia kila mwaka kutokana na kuvuta moshi wa sigara
kutoka kwa wavutaji wa sigara./Mwananchi
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments