Msanii wa Bongo Fleva anayewakilisha kundi la Tip Top Connection, Madee amesema msanii wa hip hop Bongo, Fid Q kama asingekuwa msanii angekuwa professor.
Madee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Hela’ ameiambia Clouds FM, sababu kuamini hivyo ni kutokana na upeo mkubwa wa Fid Q.
“Fid kuacha muziki ni mtu mwingine kabisa, unajua mimi nakaa nae nachati nae sana namgundua kama asingekuwa mwanamuziki angekuwa professor fulani hivi. Kwa sababu ana vitu vingi sana ambavyo akiongea unaona mbona huyo mtu yupo deep, kwa hiyo vitu vingi huwa najifunza kutoka kwake,” amesema Madee.
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email
No Comments