Kocha wa Machester City Pep Guardiola ameweka wazi kuwa hana mpango wa kumuuza mshambuliaji wake Sergio Aguero.
Ujio wa mshambuliaji wakibrazil Gabriel Jesus umeleta wasiwasi na maswali iwapo Aguero atabaki au kuondoka Man City kutokana na Guardiola kumfanya Gabriel chaguo lake la kwanza.
Hata hivyo Aguero ambaye amekuwa akipata majeraha ya mara kwa mara kiwngo chake hakikuwa kibaya msimu uliopita kwani aliifungia timu hiyo jumla ya mabao 33.
Chelsea walikuwa wanamtaka mchezaji huyo huku wakiwa tayari kutoa kiasi cha pauni milioni 75 lakini sasa wanaonekana kuhamia kwa Alvaro Morata wa Real Madrid baada ya Guardiola kusistiza kuwa mchezaji huyo atabaki Man City.
“Ni mchezaji wetu na atabakia hapa”alisema Guardiola wakati akizungumzia tetesi za mchezaji huyo kuondoka Man City.
Guardiola aliongeza kuwa Manchester City wanahitaji kusajili wachezaji wengine watatu au wanne katika kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.
Man City imekua kwenye mawindo ya kuwania saini za walinzi Danilo wa Real Madrid, Benjamin Mendy anayekipiga katika klabu ya Monaco pamoja na mshambuliaji hatari wa Arsenal Alexis Sanchez.
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments