![]() |
Uwanja wa Moruleng wenye uwezo wa kuingiza watu 20,000, upo nje kidogo ya mkoa wa Rustenburg
|
Baada ya kuwang’oa wenyeji Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali, Taifa Stars Jumatano hii watakutana na timu ya taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’ hatua ya nusu fainali mchezo utakao pigwa katika dimba la Moruleng wenye uwezo wa kuingiza watu 20,000, upo nje kidogo ya mkoa wa Rustenburg.
Rustenburg ni miji yenye baridi kali nchini Afrika Kusini ukijijenga chini ya safu za milima ya Magaliasberg katika jimbo la kaskazini magharibi.
Jotoridi hushuka mpaka nyuzi 5 lakini kwa sasa imesimamia 11 ni tofauti kubwa na jiji la Dar es salaam ambalo huchezea 28 mpaka 32!. Huu ni mtihani mwingine wa hali ya hewa kwa timu yetu.
Uwanja huu ambao utapigiwa mchezo huo wa nusu fainali ni moja kati ya viwanja vilivyotumika kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 Afrika Kusini wakiwa wenyeji.
Umaarufu wake ni kutumika kama uwanja wa mazoezi au sehemu ambayo timu ya taifa ya Uingereza walipoweka kambi katika michuano hiyo.
Zambia wana uzoefu na uwanja huo baada ya kuutumia katika hatua ya robo fainali na kuwaondoa michuanoni timu ya taifa ya Botswana kwa ushindi wa magoli 2-1 .
Safu ya ulinzi ya Taifa Stars itawabidi wawe makini na washambuliaji kama Brian Mwila toka Green Buffalo na mwenzake Justin Shonga toka Nkwazi ambao ni mwiba mkali katika timu hiyo. Ndio waliowatungua majirani zao Botswana hatua ya robo fainali.
Kuimarisha kikosi chake, kocha mkuu wa Zambia Bw. Winston Nyirenda amemuongeza mchezaji kinda wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 Boston Chundu aliyeng’ara vyema katika michuano ya kombe la dunia chini ya umri huo nchini Korea Kusini. Boston anatokea katika timu ya Nkana nchini kwao Zambia.
Mchezo wa nusu fainali kati ya Zambia na Taifa Stars umekuwa gumzo katika michuano hiyo kutokana na mafanikio ya Stars mpaka sasa kama timu waalikwa.
Kucheza mechi nne mfululizo bila kupoteza katika michuano hiyo pia wakiweka rekodi ya kutoa mchezaji bora wa mechi kila mchezo inawafanya waanze kujizolea mashabiki nchini humo licha ya mwanzo kupewa nafasi finyu hata ya kuvuka hatua ya makundi.
Golikipa Aishi Manula na viungo Erasto Nyoni na mwenzake Mzamiru Yassin wamekuwa wachezaji ambao wanazungumzwa sana katika kikosi hicho cha Salumu Mayanga kocha mzawa ambaye mpaka sasa ameiongoza timu hiyo katika mechi saba bila kuppteza.
Mara ya mwisho Zambia na Tanzania kukutana katika michuano hiyo ni Julai 5 , 1997 jijini Arusha katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid na ‘ Chipolopolo ‘ ikienda sare ya 2-2 na Taifa Stars.
Na Julia 5, 2017 Tanzania itakutana tena na Zambia katika michuano ya Cosafa huku Stars ambayo imecheza mechi 4 mfululizo bila kupoteza na kuweka rekodi ya kutoa Man of da Match kila mchezo ikisubiri kurra za Mungu iliiweze kupita katika miamba ya Chipolopolo ambayo inaonekana kupigiwa upatu wa kutinga hatua ya fainali.
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments