Saturday, July 8, 2017

thumbnail

Kaseja awapa somo wachezaji

Mlinda Mlango wa Kagera Sugar, Juma Kaseja amewataka wachezaji mbalimbali hususani magolikipa kama yeye kuendelea na mazoezi katika kipindi hiki cha mapumziko ili kuhakikisha wanalinda vipaji vyao.

Kaseja amesema licha ya kuwa katika mapumziko lakini ameamua kuendelea na mazoezi pamoja na kuwafundisha magolikipa wengine ambao bado wanahitaji kujifunza ili kuwa bora zaidi.

"Nimekuwa na utaratibu, kila kipindi cha mapumziko najipangia muda wa kufanya mazoezi, kama huwezi kujiandaa vizuri pia huwezi kucheza vizuri, kwa hiyo huu ndio utaratibu wangu, nipo na magolikipa wengine wengi ambao wanatamani kuwa kama mimi au kuliko mimi" alisema Juma Kaseja

Kaseja amesema wameona mabadiliko makubwa kwa magolikipa wanaohudhuria mazoezi hayo ambapo amewataka magolikipa wengine wajitokeze ili kuweza kujifunza kabla ya kuanza kwa Ligi mbalimbali hapa nchini.

"Mwanzo tumeanza mazoezi tulikuwa wachache lakini muda unavyokwenda wanazidi kujitokeza na tunaona wanazidi kujifunza pia, hivyo kwa muda huu ambao tunao naamini kila anayeona ananafasi anaweza akajiunga na muda ukifika kwa kila mchezaji kuelekea kwenye timu yake naamini watakuwa wamejifunza kitu" alisisitizia Kaseja.

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music