Monday, July 17, 2017

thumbnail

Korea Kusini yataka mazungumzo ya kijeshi na Korea Kaskazini

Korea Kusini imependekeza kufanyika mazungumzo ya kijeshi na Korea Kaskazini, baada ya majuma kadhaa ya msukosuko, kufuatia hatua ya Korea Kaskazini ya kufanya majaribio ya makombora.
Ikiwa mazungumzo hayo yatafanyika, yatakuwa ndiyo ya kwanza ya juu tangu mwaka 2015
Maafisa wa vyeo vya juu walisema kuwa mazungumzo hayo yatalenga kisitisha vitendo vyote vyote ambavyo huchangia kuwepo misikusuko ya kijeshi katika eneo lenye ulinzi mkali kati ya Kusini Kaskazini.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in tangu mwanzo alikuwa ameashiria kuchukua hatua ya kuleta ushirikiano wa karibu na Korea Kaskazini.
North Korean TV releases photos of Tuesday's missile launchHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKorea Kaskanzini imekuwa ikifanyia makomboa majaribio
Akitoa hotuba hivi majuzi mjini Berlin, alisema kuwa mazungumzo na Korea Kaskazini yanastahili kufanyika na kutaka muafaka kuafikiwa.
Lakini hatua za Korea Kaskazini kuyafanyia majaribio makombora likiwemo la hivi majuzi la masafa marefu, yanaenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Naibu waziri wa ulinzi nchini Korea Kusini Suh Choo-suk, aliuambia mkutano wa wanahabari kuwa mazungumzo yatafanyika eneo la Tongilgak, katika jengo la Korea Kaskazini katika eneo lisilo na ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music