Thursday, July 20, 2017

thumbnail

Mwandosya alivyowaliza wengi msibani kwa Dk Mwakyembe

Salamu za rambirambi zilizotolewa na Profesa Mark Mwandosya kwenye msiba wa mke wa Dk Harrison Mwakyembe jana, ziliibua simanzi kwa waombolezaji kwa jinsi alvyoeleza namna mama huyo alivyomuuguza alipokuwa amelazwa nchini India mwaka 2011.

Mke wa Mwakyembe, Linah alifariki dunia Julai 15 katika Hospitali ya Aga Khan alikokuwa akitibiwa na alizikwa jana wilayani Kyela, Mbeya.

Akitoa salamu za rambirambi katika mazishi hayo, Profesa Mwandosya alimkumbusha Dk Mwakyembe jinsi marehemu alivyowauguza wakiwa India.

Dk Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, aliwahi kutibiwa India kwa wakati mmoja na Profesa Mwandosya.

“Namkumbuka shemeji yangu Linah tulipokuwa tunaumwa India alitufariji sana kwa nyimbo za dini akiwa na mke wangu, hivyo kama kufa tulipaswa kutangulia sisi kwa kuwazidi umri na hata kwa kuumwa. Lakini Mungu amemchukua yeye na sisi tutafuata,” alisema Profesa Mwandosya kauli iliyomfanya Dk Mwakyembe ainamishe kichwa kwa huzuni.

Katika msiba huo ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kwamba Serikali haitasita kuwashughulikia wanasiasa wanaotoa lugha za matusi na kuleta migogoro kwenye jamii. “Tunasikitika jinsi wenzetu wanavyokengeuka na kuzungumza maneno machafu, hivyo tutawashughulikia bila kujali nafasi zao,” alisema.

Kauli ya Majaliwa ilikuja baada ya ile ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelist la Brotherhood, Rabson Mwakanani kukemea wanaotoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli kwamba vitendo hivyo vinakiuka maadili ya dini.

“Msimtukane Rais kwani mkifanya hivyo mnatutukana sisi wote ambao tulimchagua na hata kama mnataka kufikisha ujumbe kwake msitumie lugha za matusi,” alisema wakati wa mahubiri.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aliyezungumza kwa niaba ya Chadema aliwataka viongozi wa siasa kuomboleza msiba huo bila kujali itikadi.

Viongozi wengine waliohudhuria msiba huo ni Spika wa Bunge, Job Ndugai, naibu wake Dk Tulia Ackson, Waziri Mkuu mstaafu, Samwel Malecela na Naibu Waziri wa Habari, Anastazia Wambura.

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music