Monday, July 17, 2017

thumbnail

Ndikumana anakuja Yanga FC: Amissi Tambwe

Amissi Tambwe.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe ametamka kuwa Mrundi mwenzake Yusuph Ndikumana anakuja Jangwani.

Kauli hiyo, ameitoa baada ya kuwepo tetesi kuwa wakala wake amekwamisha usajili wa kiungo huyo kutokana na kutofikia muafaka mzuri na Yanga huku ikielezwa anarejea Mbao FC.

Ndikumana ni kati ya wachezaji waliokuwepo kwenye orodha ya usajili wa wachezaji wanaotajwa kwenye usajili wa timu hiyo watakaochukua nafasi ya Mzambia, Justine Zulu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Tambwe alisema akiwa nyumbani kwao katika mapumziko alikutana na Ndikumana na kumuahidi anakuja kuichezea Yanga baada ya kufikia makubaliano na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.

Tambwe alisema ujio wa kiungo huyo utaimarisha safu ya kiungo namba 6 kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukaba na kuchezesha timu.

“Ndikumana haendi popote na badala yake anakuja kuichezea Yanga msimu ujao wa ligi kuu. Yeye mwenyewe aliniambia tulipokutana nyumbani Burundi wakati wa likizo na kuzungumza mambo mengi.

“Kikubwa aliniahidi kutua kuichezea Yanga baada ya kufikia muafaka mzuri kati ya wakala wake na viongozi wa Yanga, ninaamini ujio wake utaiimarisha timu yetu,” alisema Tambwe.

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music