Wednesday, July 19, 2017

thumbnail

Peter Msechu afungukia mapenzi yake kwa Alikiba


Msanii Peter Msechu ametaja sababu zinazopelekea kumpenda na kumkubali zaidi msanii Alikiba kuwa ni pamoja na uwezo wa msanii huyo kuimba 'live' na band.

Peter Msechu amesema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio na kusema kwa Tanzania wasanii anaowakubali zaidi ni pamoja na Amini, Barnaba Classic, Vanessa Mdee pamoja na Alikiba.

"Nampenda Amini, Barnabas Classic, katika wadada nampenda, Vanessa Mdee ila nampenda sana Alikiba kwa maana kwamba jinsi anavyoimba na 'live band', unajua mimi ni mtu wa 'live' kwa hiyo napoona msanii kwa steji anafanya show ya 'live' na kutupa kitu ambacho hakipo kwenye CD mimi napenda sana. Kwa hiyo kuna wasanii wa aina kadhaa, kuna wasanii wa studio ambao wao kufanya 'live' hawawezi lakini akienda studio mashine inamsaidia kumrekebisha lakini yupo msanii mwingine anafanya live na muziki unakuwa mzuri bila msaada wa vyombo" alisema Peter Msechu

Mbali na hilo Peter Msechu anasema kitendo cha msanii kufanikiwa na kupata jina kubwa au kutopata jina kubwa, nyimbo za msanii ku 'hit' au kuto 'hit' ni jambo ambalo yeye anamuachia Mungu ila anaamini msanii ambaye anaweza kupanda stejini na kufanya muziki bila kutumia CD ndiyo msanii mkubwa na msanii bora kwa upande wake.

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music