Mlinda mlango wa Manchester United Sergio Romero amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye mskani yake makuu Old Trafford mjini Manchester.
Mlinda mlango huyo kutoka nchini Argentina, amekubali kusaini mkataba mpya ambao utamuwezesha kuitumikia Man Utd hadi mwaka 2021.
Romero mwenye umri wa miaka 30, alijiunga na Man Utd mwaka 2015, lakini amekua akipata wakati mgumu wa kuwania nafasi ya kucheza mara kwa mara, kutokana na uwepo wa mlinda mlango kutoka nchini Hispania David De Gea.
Hata hivyo tetesi za kuwepo kwa mazungumzo kati ya viongozi wa Real Madrid na Man Utd kuhusu uwezekano wa kuondoka kwa De Gea, kunatajwa kuwa chanzo cha mashetani wekundu kuingia makubaliano mapya na Romero.
Romero ameshaitumikia Man Utd katika michezo 28, kati ya hiyo michezo sita ni ya ligi ya England.
“Sergio ni mlinda mlango mahiri na mwenye uweledi. Amekua na mahusiano mazuri na wachezaji wenzake tangu alipofika hapa, na msimu uliopita alichangia mafanikio yetu ya kutwaa ubingwa wa Europa League,” amesema meneja wa Man Utd Jose Mourinho.
“Sergio alistahili kupewa mkataba mpya, na tunajivunia kuendelea kuwa naye kwa ajili ya misimu kadhaa inayokuja.”
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments