Friday, July 21, 2017

thumbnail

Wakulima msikubali kuuza mazao ovyo – Waziri Mkuu


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kusimamia biashara ya mazao mbalimbali katika maeneo yao ili wakulima waweze kupata tija huku akiwataka wakulima kutokubali kuuza mazao ovyo.
Waziri Majaliwa ametoa agizo Alhamisi hii wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilasilo kilichoko katika mpaka wa mkoa wa Mbeya na Songwe alipokuwa njiani kuelekea wilayani Songwe kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Alisema kwa sasa bodi hiyo inazunguna nchini kote kutafuta taarifa za bei za mazao ili kubaini bei zinazotumiwa na wanunuzi wa mazao hayo kama zinastahili baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakulima wa eneo hilo.
“Wakulima msikubali kuuza mazao ovyo, wekeni na akiba ya chakula. Pia Bodi ya Mazao Mchanganyiko itakuja hapa kwa kuwa sasa inapita sehemu mbalimbali kupata taarifa za bei za mazao pamoja na kuwatafutia masoko yenye tija,”alisema Waziri Majaliwa
Pia Waziri Mkuu aliwaagiza watu wote wanaohusika na suala la usambazaji wa pembejeo kuhakikisha wanazifikisha kwa wakulima katika kipindi kisichopungua muda wa miezi miwili kabla ya kuanza kwa msimu ili kuwaondolea changamoto ya uchelewashwaji wa huduma hiyo
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Bi. Chiku Gallawa alitaja changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya kilimo ni kutokuwepo kwa soko la uhakika la mazao pamoja na uingizwaji wa pembejeo zisizofaa katika mkoa.

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music