Sunday, November 19, 2017

Wednesday, November 15, 2017

thumbnail

Magufuli aagiza jengo la Tanesco liwekewe X


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemwagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuweka alama ya X kwenye jengo la Shirika la Umeme (Tanesco) na sehemu ya jengo la Wizara ya Maji na Umwagiliaji ili kupisha ujenzi wa daraja la juu katika eneo la Ubungo (Ubungo Interchange).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumatano baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitokea Chato alikokwenda baada ya kumaliza ziara ya siku tatu nchini Uganda.

Amewataka Tanroads kuwapa taarifa wahusika kuhusu kubomolewa kwa majengo yao ili wapate eneo la kutosha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo unaolenga kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam.

“Sasa mimi nataka ikiwezekana leo au kesho muweke X jengo la Tanesco…muweke X sehemu ile ya mwanzo ya Wizara ya Maji,” amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa na wananchi waliojitokeza katika eneo hilo.

Kiongozi huyo Serikali amesema kwamba Sheria ya Hifadhi ya Barabara ilianza tangu mwaka 1932, ikafanyiwa mabadiliko mwaka 1959, 1964 na 1967.

“Sheria ni msumeno, Serikali ikifanya kosa inasulubiwa, Rais akijenga kwenye Road Reserve (hifadhi ya barabara) anachukuliwa hatua hizo hizo,” amesema Rais Magufuli wakati wa ziara hiyo.

Wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, Rais Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi wakati huo aliagiza kubomolewa kwa jengo la Tanesco, hata hivyo, aliyekuwa waziri mkuu, Mizengo Pinda alizuia kubomolewa kwa jengo hilo na mengine yaliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara.
thumbnail

Babu Tale: Najiandaa kisaikolojia kwenda jela

Dar es Salaam. Wakati siku 14 zilizotolewa na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart & Co Ltd, kwa wakurugenzi wa kampuni ya Tip Top Connection Limited kutekeleza amri ya Mahakama zikikaribia kuisha, Hamis Taletale (Babu Tale), amejitetea huku akidai kuwa anajiandaa kisaikolojia kwa kifungo.

Babu Tale ambaye pia ni meneja wa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnum, pamoja na nduguye Iddy Taletale ni wakurugenzi na pia wanahisa wa kampuni hiyo.

Februari 18, 2016, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliiamuru kampuni hiyo kumlipa fidia ya Sh250 milioni Mhadhiri wa Dini ya Kiislam Sheikh Hashim Mbonde, kwa kutumia kibiashara mahubiri yake bila ridhaa wala makubaliano.

Babu Tale amekiri kupokea taarifa hiyo ya Yono, lakini akasema kuwa yeye hajui chochote kuhusu madai hayo, kwani hakuwahi kujihusisha  na kampuni hiyo na kwamba hana cha kufanya bali anawasubiri kuona Yono hizo siku walizopewa ili waone hatua zitakazofuata.

“Lakini mimi nasema sijamdhulumu huyo mzee wala sijawahi kufanya naye biashara. Kwa kuwa hiyo ni amri ya Mahakama sawa sina cha kufanya, kama watasema tulipe nitaeleza uwezo wangu maana mimi sina uwezo huo wa kulipa hizo Sh250 milioni,” amesema na kuongeza:

“Kwa hiyo cha kufanya ni kujiandaa tu kisaikolojai hata kama ni kufungwa, kwani hata kina Mandela (Nelson) walifungwa jela hivyo hivyo.”

Amesema kuwa kampuni hiyo ilifunguliwa na ilikuwa ikimilikiwa na kaka yao Abdul Taletale (marehemu kwa sasa) kwa asilimia miamoja na kwamba baada ya kufariki kampuni hiyo haikuendelea na mali zake zote zilipotea kwani zilidhulumiwa.

Amesema kuwa japo anatajwa kama mhusika lakini hakuwahi kuwa mkurugenzi, mwanahisa wala kujihusisha kwa namna yoyote na kampuni hiyo na kwamba  hakuona taabu kwani hakujua kama kuna siku yatatokea matatizo kama haya.

Ameongeza kuwa alifahamu kuwepo kwa kesi hiyo baada ya kaka yao kufariki, ambapo wakili wa mdai alimpigia simu akimtaka afike mahakamani, lakini yeye alipuuza kwa kuwa alijua si mhusika.

Kwa mujibu wa hukumu ya kesi ya msingi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, Juni 6, 2013 Sheik Mbonde aliingia makubaliano na kampuni hiyo, kutumia kazi zake za mawaidha, kwa kuzalisha, kurekodi na kuzisambaza na kugawana faida ya mauzo.

Hata hivyo, baada ya kukamilisha kurekodi masomo saba, kampuni hiyo ilimkatia mawasiliano hadi alipobahatika kukutana na ofisa mmoja wa kampuni hiyo,  Adam Waziri ambaye alimweleza kuwa wamesitisha mpango huo.

Lakini Agosti 9, 2013, wakati mdai akiendesha mhadhara Bahi Dodoma, alibaini kuwa DVD za masomo yake zilikuwa zikiuzwa sokoni Dodoma na katika  mikoa mbalimbali, bila ridhaa yake wala makubalino ndipo akafungua kesi hiyo.
thumbnail

Malaria yamlaza Tshishimbi akosa mazoezi, Tambwe arejea

WAKATI mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe amefanya mazoezi mepesi leo, kiungo Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi hakutokea kabisa.

Yanga SC imefanya mazoezi leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City Jumapili.

Tambwe ambaye hajacheza kabisa msimu huu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti, alikuwepo leo na kufanya maozezi ya kukimbia pole pole na kunyoosha viungo.

Majeruhi mwenzake, kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko hakuwepo kabisa, sawa na wachezaji wote waliokuwa na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars nchini Benin.

Tshishimbi naye hakuwepo leo na Daktari wa timu, Edward Bavu akasema kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Mbabane Swallows ya Swaziland anasumbuliwa na homa ya Malaria.

Bavu alisema Tshishimbi anaweza kurudi mazoezini kesho sambamba na wachezaji waliokuwa na Taifa Stars nchini Benin. 

Taifa Stars imerejea nchini alfajiri ya leo kutoka Benin ambako Jumapili ilitoa sare ya 1-1 na wenyeji katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa l'Amitie, au Urafiki mjini Cotonou ambao ulionyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Azam.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa wa nchini humo, Ligali Praphiou aliyesaidiwa na Bello Razack na Koutou Narcisse, hadi mapumziko wenyeji The Squirrels, walitangulia kwa bao la la penalti ya utata ya Nahodha wao, Stephane Sessegnon kipindi cha kwanza, kabla ya Elias Maguli kuisawazishia Stars kipindi cha pili.

Thursday, August 17, 2017

Friday, July 21, 2017

thumbnail

Yajue ‘mahaba’ ya Vanessa Mdee kwa Patrice Evra na Zlatan Ibrahimovic


Msanii wa Bongo Flava, Vanessa Mdee ameeleza sehemu ya pili ya maisha yake katika michezo kwa kusema yeye ni shabiki mkubwa wa Manchester United.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kisela’, amekiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm kuwa tangu high school alikuwa mpenzi wa mpira wa miguu na ndio sababu ya kuwa shabiki wa Man United pia kuna wachezaji wanamvutia zaidi katika klab hiyo.
“Ndiyo kuna wanaonivutia, nampenda sana mchezaji mmoja anaitwa Patrice Evra hasa sasa hivi namfuatlia kwenye mitandao ya kijamii zamani alikuwa anaichezea Man United sasa hivi amehama anachezea timu flani hivi, page yake ya instagram ni ya kuvutia na kuhamasha vijana, very positive, so his my favorite right now, lakini zaidi nampenda Zalatan Ibramovich,” amesema Vanessa.
thumbnail

Msanii Chester Bennington afariki dunia kwa kujiua


Chester alikutwa amefariki dunia akidaiwa kujinyonga mwenyewe nyumbani kwake Palos Verdes Estates mjini Los Angles. Muimbaji huyo wa Linkin Park pia alikuwa na urafiki wa ukaribu na Chris Cornell amabye na yeye alijiuwa mwezi Mei mwaka huu kwa kuzidisha madawa.
Joe Hahn DJ wa kundi la Linkin Park akielekea msibanit
Chanzo cha kifo cha Chester kimeelezwa kuwa marehemu alikuwa akinyanyaswa na mwanaume mmoja hali iliyokuwa ikimpelekea kujiona kama mtoto.
Kifo hiko kimetokea wakati kundi la Linkin Park, likijiandaa kwenda kufanya photoshoot mjini Hollywood kwa ajili ya wimbo wao mpya. Marehemu ameacha watoto sita aliokuwa amezaa na wanawake wawili tofauti, pia inaelezwa msanii huyo alikuwa akitumia madawa ya kulevya pamoja na pombe kali.
thumbnail

HALI ya Mchekeshaji Mzee Majuto sio Nzuri...Anaitaji Maombi yako


MWEZI Mei, mwaka huu, gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda liliripoti habari mbaya juu ya lejendari wa vichekesho Bongo, Amri Athman ‘Mzee Majuto’ kuwa katika hali mbaya kiafya, lakini kwa hali yake ilivyo kwa sasa anahitaji dua za Watanzania.

AFANYIWA UPASUAJI
Habari mbaya zilizolifikia Amani, mapema wiki hii zilieleza kuwa, Mzee Majuto yu kitandani kwa mara nyingine kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa uliosababisha afanyiwe upasuaji.
Chanzo makini kililieleza Amani kuwa, Mzee Majuto ambaye amezaliwa mwaka 1948, alilazwa kwa siku tano hospitalini huko mkoani Tanga akisumbuliwa na ugonjwa wa hernia (ngiri) ambapo ililazimu afanyiwe upasuaji ili kumsaidia kwenye tatizo lake hilo la muda mrefu.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, kufuatia tatizo hilo, Mzee Majuto amekuwa akitumia dawa za hospitalini na zile za kienyeji, lakini hakuna unafuu wowote anaoupata.
“Kuna kipindi alilazwa hapo katikati, alipopata nafuu aliruhusiwa lakini wiki iliyopita alibanwa sana na unajua yule mzee alikuwa anaogopa kufanyiwa operesheni ila kutokana na afya yake imebidi akubali tu,” kilisema chanzo chetu hicho na kuongeza:
“Kimsingi Mzee Majuto anahitaji dua za mashabiki wake na Watanzania kwa jumla.”



MKE WA MZEE MAJUTO AFUNGUKA
Baada ya kupata habari hizo, Amani lilimtafuta msanii huyo kwa njia ya simu yake ya kiganjani ambapo ilipokelewa na mkewe, Aisha Yusuf ambaye alithibitisha mumewe kuumwa.

Mama Majuto alisema kuwa, hadi wakati anazungumza na gazeti hili alikuwa yupo na mumewe katika Hospitali ya Tanga Central Health Centre (TCHC) ambako alilazwa kwa siku tano na kufanyiwa upasuaji.

“Ni kweli Mzee Majuto anaumwa ndiyo maana nimepokea simu yake, nipo naye hapa hospitalini, anasumbuliwa na ugonjwa wa hernia ambao umeibuka na kumuanza tena.
“Tunamshukuru Mungu kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji hivyo Watanzania na mashabiki wake waendelee kumuombea na Mungu akipenda hivi karibuni tu atarudi mzigoni, watarajie mambo mazuri kutoka kwake,” alisema mama Majuto.

Amani lilipoomba kuzungumza na Mzee Majuto mwenyewe, mkewe alisema alikuwa usingizini kwani alitakiwa apumzike baada ya upasuaji.
“Nitamfikishia pole lakini haruhusiwi kuzungumza, anatakiwa kupumzika,” alisema mama huyo na kuongeza:
“Hata hivyo, tumeambiwa tutaruhusiwa kutoka hapa hospitalini muda wowote.”

MASHABIKI WAMMISS
Wakiongea na gazeti hili, baadhi ya mashabiki wa staa huyo walisema kuwa, wamemmiss sana kwenye fani yake ya uigizaji na kumuomba Mungu afanye miujiza na amrejeshee afya yake.
“Kwa kweli tumemmiss sana, tunaamini atapona na kurejea kwenye hali yake ya kawaida,” alisema mmoja wa mashabiki aliyejitambulisha kwa jina la Said Juma.

UGONJWA WA HERNIA
Hernia au ngiri ni aina ya ugonjwa ambao humpata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo (organs) fulani kupoteza uimara au kuwa na uwazi (opening) hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo.

Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu kupata hernia ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua.
Pia kuharisha au kuvimbiwa (constipation). Vitu hivyo humfanya mtu apate hernia ambayo husababisha afanyiwe upasuaji ili kumaliza tatizo hilo.

Stori: GLADNESS MALLYA, DAR
thumbnail

Wapinzani Kenya wapigwa chini Mahakamani kuhusu karatasi za kura


Umoja wa vyama vya upinzani wa National Super Alliance (Nasa) nchini Kenya umepata pigo baada ya kesi yao ya kupinga zabuni ya karatasi za kupigia kura kupewa kampuni moja ya Dubai kutupiliwa mbali na Mahakama Kuu.
NASA walifungua kesi katika mahakama kuu dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ikipinga uamuzi wake wa kuipa zabuni ya kuandaa karatasi hizo kampuni ya Al Ghurair iliyoko nchini Dubai kwa madai kuwa haikufuata taratibu za manunuzi ya umma na kwamba ililenga kuwafaidisha umoja wa chama tawala wa Jubilee.
Jopo la majaji watano wa Mahakama kuu liliamuru zabuni hiyo kuendelea kwa njia ya manunuzi ya moja kwa moja kwa kuipa kampuni ya Al Ghurair bila kufuata utaratibu wa kutangaza zabuni na kuingia katika ushindani.
“Tumebaini kuwa njia ya kufanya manunuzi moja kwa moja iliyotumiwa na IEBC haikuwa na nia ya kuepuka ushindani bali ilitokana na ufinyu wa muda kuelekea tarehe ya uchaguzi,” ilieleza sehemu ya hukumu hiyo.
Mahakama Kuu iliongeza kuwa zabuni hiyo ya karatasi za kupigia kura haiwezi kugawanyika kwani ni ya aina moja, hivyo njia ya ushindani haikuwa na ulazima na kwamba sababu za IEBC zilikuwa na mashiko.
Kesi hiyo ilifunguliwa na NASA ambao waliiomba Mahakama Kuu kufuta mpango wa kufanya manunuzi ya karatasi hizo moja kwa moja kwa Al Ghurair.
Nasa wakuwa wakilalamika majukwaani kuwa wana mashaka na uhusiano kati ya wamiliki wa kampuni hiyo na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa serikali ambao wako katika kambi ya Jubilee.
thumbnail

Umesikia kauli ya Chaz Baba?

Msanii wa muziki wa dansi, Chaz Baba.

Msanii wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Chaz Baba amefunguka kwa kudai muziki wa dansi hawezi kufa kama wasanii wake wangali wapo hai huku akisisitiza kwamba na kama ukifa basi heshima ya 'Live band' itaendelea kuwepo.

Chaz Baba amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoa EATV baada ya kuwepo imani ya kwamba muziki wa dansi umekufa  nchini Tanzania kutokana na kutosikika kwa muda mrefu wasanii wake wakiwa wanatumuiza katika majukwaa ya burudani.

"Wengi wanasema muziki wa dansi umekufa lakini nasema kuwa hakuna wakuua muziki wa dansi ikiwa wanamuziki wenyewe bado wapo hawajakufa, pengine labda wanamuziki wote wa dansi wakifa ndiyo utakapokufa muziki wenyewe", amesema Chaz Baba

Pamoja na hayo, Chaz Baba aliendelea kwa kusema "isitoshe pia, utaoa muziki wa dansi lakini heshima ya muziki wa 'Live' ubaki hata kwa wenzetu walioendelea 'play back' hakuna muziki ni 'Live' tu kwa hiyo ndiyo maana sisi waasisi tupo na wazima wa afya", amesisitiza Chaz.

Kwa upande mwingine, Chaz Baba amewataka wasanii wenzake waendeleze umoja wao waliyokuwa nao kipindi cha nyuma katika kushirikiana kazi zao za sanaa pamoja na kujitokeza endapo wamepata mualiko wa kufanya mahojiano na vyombo vya habari.
Mtazame hapa anavyofunguka mengine zaidi.

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music