Habari za muda huu
mpendwa wangu, bila shaka u zima wa afya tele kabisa, kama ipo hivyo
nashukuru sana, japo mimi afya yangu
haipo vyema, ila hainizuii kuleta kusudio langu ambalo nimelipanga kusema nawe
siku ya leo. Na siku ya leo nataka tuzungumze jambo moja amabalo limekuwa ni
kikwazo sana katika maisha yetu kwa ujumla. Na jambo hili hili limekuwa
likileta majuto sana hapo baadae.
Jambo hili si jambo
jambo geni bali ni jambo ni utumwa wa fikra. Utumwa wa fikra zetu ndio adui
namba moja wa maisha yetu naweza nikasema hivyo, kwa sababu tumeshindwa
kutambua mchango sahihi wa fikra zetu, hata kupelekea kukosa uhuru wa kifkra na
kuwa ni watumwa wa fikra.
Utumwa wa fikra
huanza katika kuwaza hadi kutenda. Wengi wengi tumekuwa ni watu legelege sana
katika kutenda mambo ya msingi. Wengi tumekuwa tukiwaza waza juu juu tu katika
kuwaza. Kutokona hali hiyo ndipo nipojumuika na yule ambaye alisema katika
dunia hii hakuna kazi ngumu kama kazi ya kufikiri.
Aliyesema hivyo nafikiri
alikuw yupo sahihi, kwa sababu tumekuwa watumwa wa fikra zetu. Wengi tumekuwa
tukiongozwa na akili zetu, badala ya sisi kuziongoza akili zetu. Wengi tumekuwa
tukikurupuka katika kuchukua maaumizi ya ghafla pasipo kutafakai, na kitendo
hiki huja kuwa majuto mbeleni.
Siyo hilo tu, utumwa
wa fikra zetu umeegemea zaidi katika kuambiwa zaidi, fanya hiki fanya kile,
sisi tumekuwa na wapewa maaumuzi zaidi, kuluko kutoa maaumuzi. Najaraibu kuwaza
kwa sauti hivi kweli tumeshindwa kuamua katika maisha yetu mpaka mtu mwingine
afanye maaumuzi juu ya maisha yetu? Nawaza nakosa majaibu.
Kushindwa kuwaza
vyema juu ya maisha yetu kumetufanya tushindwe kufanya mambo ya msingi ambayo
tunayataka. Na kufanya mambo tusiyoyapenda ni utumwa wa fikra ambayo ni njia
ambayo husaidia kulekea umaskini.
Hivyo ili uweze kuepukana na utumwa wa fikra
ingefaa ufanye mambo yafuatayo;
1.
Jipe
nafasi ya kuwaza kuhusu maisha yako kwa kujiuliza maswali yafuatayo?
-unataka nini?
- unataka kufanikiwa katika jambo lipi?
- unataka kutimiza jambo hili kwa njia zipi?
- ni nani atakuwa msaada kwako.
Ukishapata majibu juu ya maswali hayo jaribu
kutafuta majibu ya kweli, na majibu ya kweli haya ni vyema ukayafanyia kazi.
Lakini mwisho kabisa hakikisha unatafuta kitu ambaho unachokipenda zaidi ndo ukifanye.
Kwani kufanya kitu ambacho unakipenda ndiyo njia sahihi ya kuondoka katika
kifungo cha umaskini.
By afisa mipango; Benson Chonya
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments