Imebainika sababu ya kundi la Yamoto Band kuamua kila msani kutoa wimbo wake ni baada ya msanii Aslay kutoa wimbo ‘Kida’ bila ruhusa ya uongozi wa kundi hilo na bila kushauriana na wenzake.
Yamoto Band
“Kile kitu kilifanya tujiulize kwa nini huyu katoa ngoma sisi wengine tukikaa kimya tutaonekana kama hatuna uwezo wa kufanya kitu, ebu nasisi tufanye lakini hatukutaka kufanya kama alivyofanya yeye, basi tukaomba uongozi wetu na kukubaliana, Mkubwa akasema mnakuwa mnajiongeza na kujikuza kwenye muziki,” amesema Beka.
Beka ameongeza kuwa zamani watu walikuwa wanawaomba kila mmoja atoe wimbo wake lakini kwa wakati huo walishindwa kujibu maombi yao.
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments