Ukisikia neno kufanikiwa
, katika akili yako kwa harakaharaka huwa kinakujia nini? Maana watu wengi
tumekuwa hatafahamu juu ya neno kufanikiwa. Wengi wetu hudhani ya kwamba neno
kufanikiwa, ni mafanikio yako binafsi tu, hivyo ndivyo ambavyo wengi wetu
hudhani.
Lakini ukweli ni kwamba
ili yaitwe mafanikio ni lazima kufanikiwe kwako kuwe na matokeo chanya kwa watu
wengine, huwezi sema umefanikiwa kama jamii na watu wengine waliokuzunguka
wakiwa bado katika shida,hayo siyo mafanikio.
Ila mafanikio ni ile hali
ya wewe kuweza kuwasaidia watu wengine
pia, huko ndiko tunakosema kufanikiwa. Wengi wetu tumekuwa wabinafsi sana
katika mambo yetu mbalimbali tunayoyajua, tumekuwa tukiyona mafanikio katika
maisha yetu tu, lakini ukweli ni kwamba kufanya hivyo si sawa hata chembe.
ila ukweli ni kwamba neno
kufanikiwa ni lazima kuwe na mahusiano ya wazi baina yako na watu wengine.
Jaribu kuchukua dakika chache kisha uwaze je watu wengine wamekuwa wakinufaika
nini kutoka kwako? Usinipe jibu. Kwa maana majibu unayo wewe.
Ila naomba nikusisitize
kwa kusema ya kwamba jijingee nafasi ya kuwasaidia wengine kama unataka
kufanikiwa zaidi, kwani unapofanya hivyo, ndivyo ambavyo unavyopata Baraka za
kimafaniko zaidi. Kwani katika hili kuna usemi ambao husema anayetoa ndiye
anayepokea zaidi.
Hivyo kila wakati
jijengee uwezo ndani yoke kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine haijalishi ni
hali gani ambayo unayo. Najua hapo bado
njia panda kwamba nazungumzia nini? Usiajali nipo kwa ajili yako.
Ninachotaka kukwambia ni
hivi jamii inayokuzunguka ni lazima inufaike kupitia wewe, nawe utanufaika zaidi
kupitia jamii hiyo. Huwezi kusema unataka kufanikiwa wakati hauna mahusiano
mazuri na watu wengine. Hivyo kila wakati kama kweli unataka kufanikiwa jitahidi
kuwasaidia watu wengine kwa kutoa mchango wako, ili siku moja watu hao waje
watamke kwa vinywa vyao kwamba mafanikio yangu yamechngiwa na mtu fulani.
Lakini pia kufanikiwa
huenda sambamba na utoaji wa sadaka. kwani kuna mahali niliwahi soma, mwandishi
alisema ya kwamba kutoa sadaka ni kumkopesha mwenyezi Mungu,
huwezi kuema hufanikiwi wakati hutoi sadaka kwa ajili ya kuwasaidia watu
wengine. Hivyo kila wakati kama unataka kufanikiwa zaidi jitahidi kutoa sadaka
kadri uwezavyo. Na daima ili uweze kufanikiwa
yakumbuke maneno haya ya kwamba mkono unatoa zaidi ndiyo mkono upokea mara
dufu.
Hivyo jijengee mazoea ya
kutoa sadaka na kuwapa mawazo watu wengine ambayo yatawajenga kwa namna moja
ama nyinyine. Hivyo ni vyema ukafikiria na kuona na kwa jinsi gani unavyoweza
kuinufaisha jamii yako kwa hicho kidogo ilichonacho.
Mpaka kufikia hapo ndugu
yangu sina la ziada ya kusema hakikisha ya kwamba unakuwa ngao zaidi ya watu
wengine kwa kutoa mchango wako kwa namna moja ama nyingine. Nikiutakie siku njema na utekelezaji mwema.
Ni wako : afisa mipango
Benson Chonya
0757909942
dirayamanikio@gmail.com
Subscribe by Email
Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments