Wednesday, June 14, 2017

thumbnail

Uzalendo ni kufanya jambo ambalo wengi hawakuelewi – Zitto Kabwe




Baada ya siku tatu kupita tangu Rais John Pombe Magufuli apokee ripoti ya pili ya uchunguzi wa mchanga wa Madini Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amefunguka na kusema uzalendo ni kupigania vitu ambavyo watu wengi watakuona mjinga.


Zitto Kabwe ameweka picha kwenye kurasa za mitandao yake ya kijamii akiwa bungeni kipindi cha nyuma yeye pamoja na Mbunge Tundu Lissu na kusema siku zote Uzalendo ni kufanya jambo ambalo watu wengi hawakuelewi lakini wewe unajua kuwa ni jambo sahihi na unakubali kutukanwa, kusimangwa, kuzushiwa lakini wewe unaendelea kupambana.

“Mwisho wa siku historia inaandikwa tu. Uzalendo ni kufanya jambo ambalo wengi hawakuelewi lakini wewe unajua ni jambo sahihi na unakubali kutukanwa, kususubikwa, kusimangwa, kuzushiwa, lakini Unapambana tu.” ameandika Zitto Kabwe.
Hata hivyo Zitto Kabwe ameendelea kusisitiza kuwa hata kama watu watakucheka na kukuona msaliti wewe endelea kupambana ipo siku watu hao waliokuita msaliti watakuita shujaa huku wale waliokuzomea watakushangilia.

Mwisho wa siku waliokuita msaliti watakuita shujaa. Waliokuzomea wanashangilia. Wewe unafanya nini? Unakaa kimya kwani kwenye kukaa kimya pia kuna kusema kukubwa zaidi. Muhimu Nchi ifaidike. Huko nyuma nilipata kusema, hata Mungu akinichukua sasa unakwenda ukiwa umetabasamu kwani unakuwa umetimiza wajibu wako duniani“ameandika Zitto Kabwe

Subscribe by Email

Follow Updates Articles from This Blog via Email

No Comments

About

Powered by Blogger.

Facebook

STORI ZA NYUMA

DESIGNED BY: SEETHEAFRICANLINK

MICHEZO

3/SPORTS/small-col-left

HABARI

3/GENERAL NEWS/small-col-left

UDAKU

3/GOSSIP/small-col-left

BURUDANI

3/ENTERTAINMENT/small-col-left

Fashion

Nature

Business

Main Slider

10/slider-recent

Music